The Manifesto
Wito wa kuchukua hatua ili kuwashirikisha vijana wote na vijana wachanga katika tathmini
Sisi, wanachama wa jumuiya ya kimataifa ya tathmini, pamoja na serikali, wabunge, mashirika ya Hiari ya Kitalaamu ya Tathmini (VOPEs), mashirika ya Umoja wa Mataifa, watathmini, wasomi, sekta binafsi na sekta za maendeleo.
Tunatambua kwamba watathmini wachanga na wanaoibukia wanachangia kikamilifu katika kuunda utamaduni wa kimataifa wa tathmini, na wanazidisha nguvu ya mabadiliko ya tathmini ili kujenga ulimwengu endelevu, jumuishi, na wenye usawa ulioandaliwa na haki ya kijamii na usawa.
Tunakubali jukumu na wajibu wetu katika kukuza na kusaidia ushiriki wenye maana wa vijana wote na watathmini wachanga na wanaochipukia katika michakato ya tathmini na katika wahamasishaji wa tathmini, ili kusaidia kufanikiwa kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu.
Tunajitolea kufanya juhudi za kimkakati na za pamoja ili kujenga uwezo wa kitaaluma wa watathmini vijana na wanaoibukia.
Tunakubali, kukuza na kuimarisha ushiriki wa kweli na wa maana wa vijana katika tathmini, kwa kuzingatia utofauti wa vijana, kwa kushirikiana na vijana katika kubuni, maendeleo na matumizi ya tathmini. Hii ni pamoja na kushirikisha vijana wote na watathmini vijana na wanaoibukia katika awamu zote za tathmini, ikijumuisha:
-
Watoa taarifa muhimu, kutoa mitazamo na ushahidi wakati wa ukusanyaji wa data za tathmini, kwa kuweka mkazo kwa vikundi vya vijana visivyo na uwakilishi.
-
Watathmini-wenza, ambao hufanya tathmini pamoja na watathmini waandamizi.
-
Washauri, ambao huchangia maarifa kama matokeo ya mchakato wa tathmini.
-
Wafanya maamuzi, wanaosaidia kuoongoza na kutoa mwelekeo wa mchakato wa tathmini kwa kushirikiana na makamishna na/au mameneja wa mchakato wa tathmini.
-
Watetezi wa matumizi ya tathmini
Tunakubali kwamba ushiriki wa maana wa vijana, watathmini vijana na wanaoibukia katika tathmini ni mchakato unaoendelea, na si juhudi za mara moja, ambayo inahitaji kutafakari juu ya mchakato kwa kutumia mafunzo kwa ajili ya mabadiliko.
Tunaahidi kuwa mstari wa mbele kwa vijana katika tathmini!